Burudani

ITV na Clouds FM zawa Superbrand kwa mara nyingine tena!

Kituo cha runinga cha ITV na kituo cha redio cha Clouds FM kwa mara nyingine vimetunukiwa tuzo ya ubora ya Supebrand Afrika Mashariki kwa mwaka 2015/2016 vikiwa ni vituo pekee vya habari katika kundi la makampuni kumi bora katika tuzo hizo.

5
Washindi wa Superbrands 2015/2016 baada ya kutunikiwa vyeti vyao

Akipokea cheti cha Superbrand Jumatano hii, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM na Ruge Mutahaba alisema kituo hicho kitaendelea kujikita katika kuandaa vipindi vyenye ubora ili kuendelea kuwa namba moja katika matangazo ya redio.

Alisema Clouds FM imekuwa superbrand kwa mara ya tatu mfululizo lakini awamu hii imeenda mbele zaidi kwa kuibuka superbrand Afrika Mashariki. “Mafanikio haya makubwa hayakuja ndani ya usiku mmoja, lakini ni kwa kupitia kujituma na kujikita katika uandaaji wa vipindi bora na vya uhakika,” alisema Mutahaba.

_MG_0868
Kutoka kushoto: Fauzia Abdi, Ruge Mutahaba, Jawad Jaffer na Sebastian Maganga

Mutahaba alisema jitihada zaidi zitaendelea kuwekwa ili kuhakikisha kuwa vipindi vya redio hiyo vinafikia viwango vya kimataifa ili ije kuwa superbrand barani Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhaville alisema tuzo hiyo ina maana kubwa kwa kampuni yake ambayo tayari imechomoza kwenye soko la Afrika mashariki ikijipanga kujikita kwenye soko la Afrika kwa ujumla.

Pamoja na Clouds FM na ITV, makampuni mengine ya Tanzania yaliyopata tuzo hiyo ni pamoja na Alliance Insurance na Petrolfuel.

Majina hayo yalipatikana kufuatia utafiti uliofanywa na kampuni ya Superbrands yenye makao yake makuu jijini London na uliohusisha watu 600 wakiwemo wataalam wa masoko na walengwa wa bidhaa na huduma mbalimbali.

Mkuu wa Superbrands East Africa, Jawad Jaffer alisema makampuni hayo yameshinda kufuatia mchakato wa uchaguzi uliofanywa na baraza la superbrands na walengwa wa huduma na bidhaa hizo wa Afrika Mashariki.

Ubora, Uhakika na Upekee ndio vigezo vitatu vikubwa vilivyotumika kuzipata superbrands.

Zaidi ya makampuni 1000 yalishindanishwa kwa kufanyiwa utafiti wa kina na kisha kubaki makampuni 20 pekee huku jumla ya kampuni 11 zinazotoa huduma za kuzalisha bidhaa zikiendelea kubaki kwenye orodha ya 20 bora ya SUPERBRANDS.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents