Siasa

Ivory Coast: Waziri Mkuu apoteza maisha mara tu baada ya kutoka kwenye mkutano wa baraza la mawaziri

Waziri Mkuu wa Ivory Coast Amadou Coulibaly amefariki baada ya kuugua wakati wa kikao cha baraza la mawaziri. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 alikuwa amechaguliwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, baada ya Alessane Ouattara kusema kuwa hatowania muhula wa tatu.

Bwana Gon Coulibaly alikuwa amerudi kutoka Ufaransa ambapo alikuwa amepokea matibabu ya moyo kwa miezi miwili.

Rais Ouattara amesema kuwa taifa linaomboleza.

Alisema kwamba bwana Gon Coulibaly alianza kuhisi vibaya wakati wa kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri na akapelekwa hospitali ambapo alifariki baadaye.

Kifo chake kitasababisha hali ya switafahamu kuhusu uchaguzi huo.

Bwana Coulibali alifanyiwa upandikizaji wa moyo 2012 na alikuwa ameelekea Ufaransa tarehe 2 Mei ili kuwekewa bomba katika mshipa wake wa damu.

Alirudi Alhamisi iliopita na kusema: Nimerudi kuchukua mahala pangu kando ya rais , ili kuendelea na jukumu la kujenga taifa letu.

Taarifa moja katika gazeti la Le Monde siku ya Jumatatu ilimnukuu afisa mmoja wa kigeni ambaye yumo nchini humo kama mchunguzaji wa uchaguzi huo ilisema: Iwapo Gon Coulibaly hajapona, Ouattara atakuwa hana chaguo bali kuwania kwa muhula mwengine kwasababu hakuna mpango mwengine.

Suala hili kufikia sasa limekuwa mwiko kwasababu rais amesema yuko tayari kuondoka na kutaja ni nani chaguo la mtu atakayemrithi.

Chaguo la bwana Ouattara kutowania urais mwezi Machi lilishangaza taifa hilo.

Wakati huo, mwandishi wa BBC James Copnall aliandika kutoka mji mkuu Abidjan, kwamba wanasiasa walimpongeza bwana Ouattara baada ya kukataa kusalia madarakani suala ambalo sio la kawaida kwa viongozi wa eneo hilo.

Hata kufikia wakati huo, ilikuwa wazi kwamba bwana Gon Coulibaly angeungwa mkono kama mrithi wa Ouattara.

Alassane Ouattara

Key facts: Alassane Ouattara

  • Bornon New Year’s Day in 1948
  • Memberof the Islamic faith
  • MarriedFrench businesswoman Dominique Folloroux in 1991
  • PhDin economics and worked for IMF
  • Sworn inas president on 6 May 2011 after years in oppositionPresentational white space

Wafuasi wa Ouattara wanasema kwamba ameleta ukuaji wa kiuchumi, udhabiti na kuimarisha sura ya Ivory Coast katika ngazi ya kimataifa.

Lakini wanasiasa wa upinzani na raia wengi wa Ivory Coast wanasema kwamba rais huyo hakuwahudumia vya kutosha ili kuliunganisha taifa hilo na kuponya vidonda vya mgogoro mbaya ulioligawanya taifa hilo kabla ya yeye kuchukua madaraka.

Takriban watu 3,000 walidaiwa kufariki katika vita vilivyosababishwa na mgombea Laurent Gbagbo aliekataa kwamba ameshindwa uchaguzi wa 2010 na bwana Ouattara, kabla ya vikosi vinavyomtii rais aliepo madarakani kumkamata Gbagbo Aprili 2011.

Mgogoro wa kisiasa uliochukua muda mrefu kati ya bwana Ouattara na rais wa zamani , Henri Konan Bedie ulisababisha janga nchini Ivory Coast.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents