IVORY COAST: YAJIFUNIKA SHUKA ASUBUHI


Baada yakuifunga North KOREA mabao matatu kwa bila na kujikuta wakiwa nje ya michuano ya WC 2010 ijapokua ushindi, Ivory coast walionyesha kandanda safi na kuyaaga mashindano kama mashujaa.

TOURE YAYA aliwapatia Ivory coast bao la kwanza na baadaye SOLOMON KALOO akaiandikia bao lingine.

IVORY COAST wametolewa kwenye michuano baada ya kufungwa mechi moja na Brazili kutoa droo na Portugal.

Imewafanya kwenye kundi lao wawe washindi wa tatu wakati Brazil wakiwa wanaongoza kundi hilo na Portugal wakiwa washindi wa pili.

Wakati huo huo mshambuliaji nyota wa timu hiyo Didier Drogba amesema walicheza kwa kujiamini lakini bahati haikuwa yao.
Amesema japokua ni msimu wake wamwisho kuchezea timu hiyo amewapongeza wachezaji wenzake na kuwataka wawe na moyo wakati wanapo ichezea timu yao ya taifa.

Mchezaji huyo anaamini kunavipaji vingine vingi ambavyo vitajitokeza kutoka kuichezea timu hiyo

Aliwasihi mashabiki kuiombea timu ya Ghana iweze kusonga mbele kwenye mchuano wa kombe la dunia. Ghana wanaweza kusonga mbele wakiendelea kucheza kitimu kama walivyocheza mechi zao za nyuma.

Kocha wa Ivory Coast Sven Goran Eriksson amesema timu yake ilicheza vizuri japokua wametoka kwenye michuano hiyo aliendelea kusema anahitaji muda zaidi wa kukaa na timu hiyo na anaamini Ivory Coast ni timu nzuri na inaweza kufanya makubwa siku za mbele.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents