Burudani

Izzo B amshirikisha Belle 9 kwenye ngoma mpya


Rapper anayewakilisha Mbeya city, Emmanuel Simwinga aka Izzo B, siku si nyingi anatarajia kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha mkali wa chorus nchini, Belle 9.

Kwa mujibu wa Izzo B ngoma hiyo ni ya kimtaa zaidi ambayo ameamua kuifanya baada ya kufufuliza kutoa ngoma zenye mafunzo na ujumbe mzito kuhusu serikali.

Tangu atoe Rizone na baadaye kutoa mwendelezo wake kwa kuachia wimbo alioupa jina la ‘Barua’ aliomshirikisha Dully Sykes, Izzo ameendelea kuachia ngoma za aina hiyo huku ‘Mwaka Jana’ ikiwa miongoni mwa nyimbo hizo.

Amesema katika wimbo huo mpya uitwao ‘Utarudishwa ambao beat yake imetengenezwa na rapper mahiri nchini, One The Incredible umeingiziwa sauti mjini Mororgoro kwenye studio za Dirty Mode Records chini ya producer Tris.

Ameongeza kuwa kila kitu kimekamilika na sasa kinachosubiriwa ni mixing pekee ambayo inaweza kukamilika siku za hivi karibuni.

Kwenye wimbo huo, Izzo Bizness amesema amezungumza vitu vingi hasahasa kuhusu yeye na namna anavyomudu game la hip hop.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents