Burudani

Izzo Bizness awashirikisha Fid Q, Jay Moe na Shaa kwenye ngoma mpya ‘Inanichosha’

Rapper na mjasiriamali wa Mbeya, Izzo Bizness anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Inanichosha’ aliowashirikisha Fid Q, Jay Moe na Shaa.

Izzo BIZ NESS

Akiongea na Times FM, Izzo B amesema mdundo wa wimbo huo umetayarishwa na producer KTB wa Mbeya na kisha vocal na mixing zimefanywa na Master Jay.

“Kuna vitu tumeongea tu ambavyo vipo vinaendelea katika maisha, katika hii game ambavyo vinachosha, yaani kwamba habari fulani na hali fulani inayoendelea inachosha, unajua. Nafikiri ikitoka watu ndo wataelewa nini ambacho namaanisha zaidi kwa sababu utamu hatuwezi kuumaliza sasa hivi,”amesema Izzo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents