Burudani

Izzo Bizness ‘Humwambii Kitu’ tena!

Picha kutoka kwenye mtandao wa Instagram ya Izzo akiwa kwenye studio ya producer Dunga

Baada ya Utarudishwa, huenda Izzo Bizness ‘usimwambie kitu tena’! Kwanini? Don’t get it twisted, ni jina la wimbo wake alioupika jana kwenye jiko la producer aliye ‘mguu nje ndani’nchini Tanzania, Dunga wa Mandungu Digital.

Baada ya kuona picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram anayooenaka akiwa busy kupitia mistari kwenye smartphone yake ndani ya studio hizo za Dunga zilizopo nyumbani kwake, Bongo5 ilimpigia simu kutaka kujua nini anawaandalia mashabiki wake.

Izzo alisema ngoma hiyo inaitwa ‘Huniambii Kitu’ na ni project ambayo haitatoka leo au kesho. Baada ya kumuuliza kwanini jina la wimbo limekaa kishari zaidi, alijibu kwa ufupi ‘ndio dawa yao’.

Hivi karibuni Dunga ambaye ni mkenya aliproduce ngoma kadhaa za hip hop ukiwemo Manuva wa Joh Makini na mwingine aliomfanyia Lord Eyez ambazo zote zinafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya radio nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents