Burudani

Rapper J. Cole awa Baba

Rapper J.Cole na mkewe Melissa Heholt wamepata mtoto wao wa kwanza tangu kufunga ndoa mwaka 2016.

J. Cole ameyathibitisha haya kwenye mahojiano aliyoyafanya kwenye jarida la ‘The New York Times’la nchini Marekani ambaloi limeandika, ” J.Cole amepata mtoto na mke wake Melissa Heholt. Huyu ni mtoto wa kwanza kwa J Cole na mke wake, ila amesita kutoa jina na jinsia ya mtoto huyo.”

Hivi karibuni Cole atatoa makala yake kupitia HBO itakayoitwa ‘J. Cole: 4 Your Eyez Only’.

Tetesi zinaonyesha kwamba ni mtoto wa kike baada ya kusikika akiimba kuhusu kuwa na mtoto wa kike katika wimbo wake, ‘She’s Mine’, Pt. 1” na “She’s Mine, Pt. 2” kutoka kwenye album hiyo mpya ya ‘4 Your Eyez Only’

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents