Burudani

J Plus na Inspekta Seba wakutanishwa tena kwenye filamu mpya ya ‘The Foundation’

Staa wa filamu za mapigano Bongo, Jimmy Mponda aka J Plus anatarajia kuachia filamu yake mpya ‘The Foundation’ mwezi Julai mwaka huu.

IMG_4247

Filamu ya mwisho ya J Plus ilikuwa ni ‘Double J’ iliyotoka mwaka 2012 na tangu hapo amekuwa kimya. J Plus anatarajia kuachia filamu hiyo iliyowashirikisha mastaa kadhaa akiwemo Inspekta Seba aliyewahi kucheza naye kwenye filamu yas ‘Misukosuko’.

J Plus amesema, “Nategemea hii filamu ya ‘The Foundation’ irudishe heshima ya filamu za action Tanzania kama ilivyo kuwa awali.”

IMG_4338

Aidha kuna tetesi nyingi zilienea kuwa J Plus na Inspekta Seba wamekuwa hawapatani kutokana na wawili hao kutoshiriki kwa pamoja kwenye filamu kwa muda mrefu huku Inspekta Seba akiwa anatoa filamu mwenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents