Jack Wilshere aipa mkono wa kwaheri Arsenal, kutua West Ham muda wowote

Klabu ya West Ham inakaribia kumsajili mchezaji wa Arsenal, Jack Wilshere baada ya kiungo huyo kumaliza mkataba na timu yake.

Wilshere ambaye alikuwa akikipiga ndani ya klabu ya Arsenal imemaliza mkataba wake na the Gunners siku ya Jumapili na hivyo kutua West Ham kwa usajili huru.

Kiungo huyo wa Uingereza pia anawindwa na klabu ya Fenerbahce huwanda akatua kwa wagonga nyundo hao wa Uingereza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema kuwa anahitaji kuendelea kusalia kwenye ligi kuu ya Uingereza ikitoa ishara kuwa hana mpango wa kucheza nje ya nchi yake wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa mwezi Agosti.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW