Michezo

Jack Wilshere atoa yamoyoni baada ya kutotajwa ndani ya kikosi cha Uingereza

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere ameeleza hisia zake kupitia mitandao yake ya kijamii mara baada ya kukosekana kwenye kikosi cha timu taifa ya Uingereza kitakacho shiriki michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi mwezi ujao.

Wilshere hakutajwa na meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate kuwa miongoni mwa wachezaji 23 watakao shiriki michuano hiyo mikubwa kabisa upande wa soka hali iliyompelekea mchezaji huyo kuandika kuwa angekuwa na mchango mkubwa kama angejumuishwa.

Kwa hakika nimeuzunishwa mno kwakutojumuishwa kwenye kikosi cha timu yangu ya taifa kwaajili ya kombe la Dunia, nilikuwa nipo fiti na mwenyeutimamu wa mwili msimu mzima hivyo naamini ningekuwa sehemu wa wachezaji hao.

Mipatieni nafasi nitakuwa na mchango mkubwa, ingawaje naheshimu maamuzi ya meneja nawatakia kila lakheri na mafanikio kwa wachezaji wote waliyopata nafasi ya kuteuliwa.

 Siku zote nisalia kuwa shabiki wa timu ya Uingereza na nitatoa mchango wangu kwa vijana waliyotoa mchango wao kwa taifa.

Wilshere amecheza jumla ya mechi 38 ndani ya the Gunners msimu huu, Uingereza itacheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kwenda Urusi, wakati mechi hizo mbili ikiwa ni dhidi ya Nigeria dimba la Wembley Juni 2 na Costa Rica.

Michuano ya kombe la dunia inatarajia kuanza Juni 14 wakati Uingereza mchezo wake wa kwanza ikiwakabili  Tunisia kisha Panama Juni 24 naUbelgiji Juni 28.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents