Habari

Jacky Wolper adai filamu yake ya ‘AFTER DEATH’ aliyoitoa kumuenzi Kanumba ilimpa hasara ya M 28

Baada ya marehemu Steven Kanumba kufariki dunia April mwaka jana (2012), muigizaji nyota wa kike wa Bongo Movie Jacqueline Wolper alitoa filamu ya kumuenzi star huyo aliyekuwa mfano mzuri kwa waigizaji wa Tanzania, iliyoitwa AFTER DEATH.

wolper33

Akizungumza na Global Publishers, Wolper amesema kuwa alikula za uso baada ya filamu hiyo kumpa hasara.

“Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au 40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13 hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25, yaani inakatisha sana tamaa,” Alisema Wolper.

Muigizaji huyo ambaye pia hutumia aka ya Wolper Gambe ameongeza kuwa hasara hiyo imetokana na tatizo ambalo huwakuta hata wasanii wenzake wa filamu, la uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi hizo za filamu za hapa nyumbani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents