Habari

Jafarai afungua car wash


Baada ya kuendelea kutofanya vizuri kwenye ramani ya muziki nchini licha ya kutoa track kibao, Mteule Jafarai ameamua kugeukia biashara.

Hata hivyo tofauti na wasanii wengine wa Bongo Flava nchini ambao mara nyingi biashara zao hujikita kwenye maduka ya nguo, msanii huyo wa ‘Niko Busy’ amefungua Car Wash.

“Ndiyo nina mchakato wa kufungua car wash yangu ambayo itakuwa inapatikana maeneo ya mikocheni Oil com karibia na TMJ lakini nitaifungua rasmi Jumapili ijayo. Ninachoomba wasanii hata mashabiki wangu waje katika Car wash yangu ili tupeane support,” blog ya Dj Fetty ilimkariri Jafarai.

Amesisitiza kuwa pamoja na kuwa na biashara hiyo, bado ataendelea kufanya muziki kama kawaida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents