Burudani

Jaguar aingia rasmi kwenye ulingo wa siasa

Charles Njagua a.k.a Jaguar ni kati ya wasanii wa wenye mafanikio makubwa kwenye muziki na pia nje ya fani hiyo nchini Kenya.

Kitu ambacho pengine wengi kutoka nje ya Kenya hawakijui ni kwamba huyu Jaguar wa leo aliwahi kufanya kazi ya kuosha magari na vile vile ya umekanika. Hakijatosha, aliwahi kushiriki dawa za kulevya kwa kipindi kirefu.

Nyota ya Jaguar ilianza kung’aa hususan Afrika Mashariki mwaka 2011 baada ya kuachia hit song yake ‘Kigeugeu’, wimbo ambao Katu hatowahi kuusahau maisha yake yote. Ni wimbo ambao ulidumu kwenye chati mbalimbali za nyumbani kwa takriban miaka miwili. Aliishia kushinda tuzo ya nyimbo bora Afrika Mashariki kwenye tuzo za Kili Awards mwaka 2012.

Hivi sasa, muimbaji huyu amefungua ukurasa mwingine kwenye maisha yake. Baada ya fununu na uvumi kuenea tangu mwaka 2013 kwamba jaguar angejitosa kwenye siasa, hatimaye ameweza kuthibitisha hilo.

Kwa mara ya kwanza, ameiambia Msetoea Jumanne hii kwamba ni kweli amejitosa rasmi katika siasa na atagombea kiti cha ubunge cha eneo la Starehe lililopo kwenye kaunti ya Nairobi katika uchaguzi mkuu mwaka huu nchini Kenya.

Kutokana taarifa hii, Jaguar sasa anajiunga na wasanii wenzake Cannibal na Frasha wa P-unit ambao pia wameingia mzima mzima kwenye siasa. Muimbaji huyu kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Worrior’ aliomshirikisha El wa Ghana.

Na :Teddyza Agwa
Instagram @teddybway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents