Burudani ya Michezo Live

Jaguar akana shtaka la kusababisha vifo vya watu wawili

Muimbaji wa Kenya Charles Njagua Kanyi maarufu kama Jaguar Jumanne ya tarehe 11 amefikishwa katika mahakama ya Baricho iliyopo eneo la Kirinyaga baada ya uchunguzi wa ajali iliyosababishwa na gari lake kuendelea kwa muda wa takriban majuma matatu.

Jaguar alijipeleka mwenyewe mbele ya hakimu mkazi bila ya mwanasheria wake na kujibu shtaka la kusababisha vifo vya vijana wawili wa bodaboda kufuatia ajali iliyohusisha gari lake aina ya Range rover spot. Awali ilionekana kama msanii huyo alijaribu kufanya ‘cover up’ kwa kuandikisha ripoti iliyotofautiana na kile walichosema mashuhuda.

Mgombea ubunge huyo ambaye alionekana kuwa na mawazo kibao wakati wa kesi hiyo alikana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana la shilingi laki moja.
Kesi hiyo itafunguliwa tena tarehe 8 June, miezi miwili kabla ya uchaguzi.

Kwa upande mwingine, familia za waliopoteza maisha zinataka aki itendeke kwa usawa.

Sasa hivi Jaguar ana kibarua kikubwa sana na mtihani mgumu zaidi katika jitihada zake za kugombea eneo bunge la Starehe ikizingatiwa kwamba tukio hilo limempa ‘negative publicity’ kwa wingi na hadi sasa ndio sakata kubwa zaidi iliyowahi kumzunguka.

Kitu cha msingi ni yeye kuwa na njia thabiti ya kukabiliana na hali hii bila ya kujenga hisia za kutokuaminiwa na watu hususan raia wa Starehe.

Imeandikwa na: Ted Agwa
[email protected]

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW