Tupo Nawe

Jaguar amjibu Prezzo, ampa ‘ofa’ ya kutibiwa rehab bure baada ya kumdiss tena

Wiki iliyopita rapper wa Kenya Jackson Ngechu Makini a.k.a Prezzo alipokuwa kwenye mahojiano na Betty Kyalo wa KTN ya Kenya, aliulizwa kuhusu msanii mwenzake Jaguar, swali ambalo liliamsha upya beef yao.

Jaguar

Prezzo alijibu kwa kejeli kuwa Jaguar anayoifahamu yeye ni aina ya gari (kama ambavyo hua anajibu mara nyingi anapolizwa kuhusu Jaguar) akimaanisha hamfahamu mtu yeyote kwa jina hilo.

Prezzo alizidi kutia mafuta kwenye moto kwa kuongeza kuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alimpa shavu Jaguar kwa kupiga naye picha na kusema ana bahati kwasababu alianza kumfahamu Jaguar kupitia picha hiyo aliyopewa shavu na Rais ambaye amedai kuwa ni rafiki yake.

Baada ya moto huo uliowashwa na Prezzo, mashabiki wa Jaguar wamekuwa wakimsukuma amjibu Prezzo, lakini Jaguar amewajibu kuwa kama ingekuwa ni miaka mitano iliyopita ndio angeweza kumjibu lakini kwa sasa ana mambo mengi ya msingi ya kufanya, hivyo anachoweza kufanya ni kumsaidia apatiwe tiba ya rehab bure, akimaanisha zile tetesi kuhusu Prezzo kutumia dawa za kulevya.

Hiki ndicho aliandika Jaguar kwenye mitandao ya kijamii:

“A lot of people have asked that I respond to @prezzo254. If it were five years ago, I would have made time to beef around with him. As a director at Nacada, I am busy addressing issues affecting the youth in our country. What Prezzo is going through is what we are fighting. The best I can do is offer him a complimentary at one of our rehabilitation facilities in Nairobi or Mombasa. He’s free to choose where he prefers to go.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW