Habari

Jaguar anunua mjengo wenye thamani ya TSH milioni 198


Hitmaker wa Kigeugeu, Jaguar wa nchini Kenya ameamua kuonesha kuwa biashara zake zinamuingiza mkwanja mwingi baada ya mwezi uliopita kununua nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 11 za Kenya sawa na milioni 198 za Tanzania.
Nyumba hiyo ipo karibu na Karen jijini Nairobi.
Msanii huyo amesema sasa ameamua kuwekeza kwenye mijengo ya biashara yaani ‘real estate’.
Amegundua kuwa muziki una muda wake ambapo anaweza kuchuja muda wowote hivyo kupanga kuwekeza kwenye mijengo kabla hajachelewa.
Kuashiria kuwa bado ataendelea kutengeneza hela zaidi kupitia muziki wanasiasa kadhaa wameonesha nia ya kutaka kuununua wimbo wake mpya uitwao ‘Matapeli’ kwaajili ya kuutumia kwenye kampeni zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents