Habari

Jaguar anunua Range Rover Sport mpyaaaaa!!


Wakati bado mashabiki wa muziki Afrika Mashariki wakijiuliza nani mwenye mshiko zaidi kati ya Jaguar na Prezzo, Jaguar ameamua kuwaonesha kuwa kuchomoa shilingi milioni 160 na ushee (Tshs) kununua mkoko ni jambo dogo sana kwake!

Mtandao wa Ghafla wa Kenya umeripoti kuwa mwanamuziki huyo wa Kigeugeu amenunua Range Rover Sport mpya na hivyo kuongeza idadi ya magari kwenye parking ya nyumba yake.

Mchizi ameonekana jana na gari hiyo yenye rangi ya ‘silver metallic’ akicruise kwenye barabara ya Uhuru jijini Nairobi.

Gari yenyewe bado mpya sana kiasi cha kutokuwa na namba.

Pengine jibu unaweza ukawa nalo tayari kama una mashaka ni nani mwenye ‘cheda’ zaidi katika Prezzo na Jaguar.

Kwamba, wakati Prezzo anazisotea dola laki tatu za Big Brother Africa, Jaguar huku anachomoa zaidi ya shilingi milioni 150 kununua miongoni mwa ndinga kali zinazokimbiza town!

Salute kwa Jaguar, hela anayo aiseee!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents