BurudaniDiamond Platnumz

Jaguar awapoteza Diamond na Davido katika mpambano wa video zao mpya ‘Kioo’ na ‘Number 1 RMX’

Wiki hii zipo video nyingi zilizotoka za wasanii wa Tanzania na Kenya, lakini zilizovutia na kuchukua vichwa vingi vya habari katika mitandao ya nchi hizo mbili ni ile video iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya Diamond Platnumz aliyomshirikisha nyota wa Nigeria Davido ‘Number 1 RMX’, na kwa upande wa Kenya ni ya Jaguar ‘Kioo’.


Video ya Platnumz ilifanyika nchini Nigeria chini ya director anayeaminika kuwa mkali zaidi Afrika Clarence Peters wa Capital Dreams, huku ya Jaguar ikiwa imefanyika Kenya chini ya director Enos Olik.

Baada ya video hizo mbili kutoka, mtandao wa GHAFLA wa Kenya uliweka mpambano wa video hizo watu waipigie kura moja kati ya ‘Number 1 RMX’ na ‘Kioo’, na matokeo yanaonesha kuwa video ya Jaguar imepata ushindi wa asilimia 75.2 huku video ya Diamond ikiachwa na asilimia 24.8 katika jumla ya kura 161 zilizopigwa.

Mpaka sasa video ya Jaguar ‘Kioo’ imetazamwa mara 63,986 toka iwekwe Youtube Jan 5, 2014 huku video ya ‘Number 1 RMx’ ya Diamond imetazamwa mara 174,157 toka iwekwe Jan 6, 2014.

Tazama video zote mbili hapo juu halafu weka maoni yako hapo chini kama ungepata nafasi ya kupiga kura ungempa nani ushindi?

Source: GHAFLA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents