Burudani

Jaguar: Ntamshukuru AY milele kwa kukubali kufanya collabo nami kipindi hakuna mtu anayenifahamu!

Kwa mujibu wa Jaguar, bila AY, hakuna mtu ambaye leo hii angekuwa analifahamu jina lake.

10838552_968130043199762_1474877217_n

Muimbaji huyo wa Kenya, amedai kuwa AY alikubali kufanya naye ngoma kipindi ambacho hakuna mtu aliyekuwa akimfahamu wala kumchukulia serious.

Jaguar alimshirikisha AY kwenye wimbo wake ‘Nimetoka Mbali’

“Will Always Be Grateful To This Guy Ay @Aytanzania For Accepting Do A Collabo With Me When Nobody Knew Me….Tuzidi Kuvuka Boda,” Jaguar aliandika jana kwenye Instagram kwa kuweka picha hiyo juu ya AY.

“Tuko Pamoja ndugu yangu,nafurahi kuona mafanikio yako sana,Huu Mwaka ufanikiwe zaidi na zaidi,” alijibu AY.

Nimetoka Mbali ndio wimbo uliomtambulisha Jaguar Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents