Burudani

Jaji atengua makubaliano yaliyoamriwa kwenye talaka ya staa wa Empire, Terrence Howard

Makubaliano ya kifedha na mali yaliyokuwa yameamriwa kwenye talaka ya muigizaji wa tamthilia ya Empire, Terrence Howard na mke wake wa pili yametenguliwa.

Terrence-Howard-Michelle-Ghent

Jaji huyo alibaini kuwa muigizaji huyo alilazimika kutoa talaka hiyo kwa vitisho vya kuvujishwa kwa mambo yake ya siri.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa Howard na mke wake wa zamani, Michelle Ghent watatakiwa kufanya mazungumzo upya ya vigezo vya kifedha kuhusiana talaka yao.

Pia uamuzi huo unayazima madai ya Ghent ya kutaka kupokea sehemu ya malipo ya Howard kutoka kwenye tamthilia ya Empire.

Howard aliitoa talaka hiyo mwaka 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents