Tupo Nawe

Jaji Mkuu Kenya adai kufanyiwa figisu ili atolewe madarakani, ‘Wametupunguzia bajeti, Hadi kununua mafuta tunashindwa’

Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga ametishia kususia kufanya majukumu yake ya kikazi, Baada ya kupunguzwa kwa bajeti ya mahakama nchini humo.

David Maraga na Rais Uhuru Kenyatta

Akiongea jana kwenye mkutano wa majaji na viongozi mbalimbali wa kiserikali nchini humo, David Maraga amesema kuwa serikali inaingilia kati utendaji kazi wa mahakama kwa kupunguza bajeti ya mahakama.

Hivi karibuni serikali ya Kenya ilipunguza zaidi ya dola milioni 30 kutoka kenye bajeti ya mwaka ya sekta ya mahakama , hatua ambayo Bwana Maraga anadai inalenga kudhibiti utendaji kazi wa Mahakama.

Jaji Maraga ambaye alionekana mwenye hasira katika hotuba yake hiyo,  amedai kinachofanywa na serikali ni njama za serikali za kumuondoa madarakani kabla ya tarehe 31 Disemba mwaka huu.

Baadhi ya mawaziri wanasema nitaondoka madarakani kabla ya mwisho wa mwaka huu , Kumbe Kenya hii ina wenyewe na sio sisi,” amesema Maraga.

Jaji huyo Mkuu wa Kenya amedai kuwa ofisi yake haiwezi hata kupata bajeti zilizoidhinishwa, na kwamba mahakama inahangaika kupata huduma muhimu kama vile Wi-Fi na mafuta ya gari.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW