Tupo Nawe

Jamaa achukuliwa mke wake kisa mechi ya Simba SC vs Yanga SC, Haji Manara aingilia kati

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba SC vs Yanga hapo jana Februari 16, 2019 jioni, Shabiki maarufu wa Yanga aitwaye, Jimmy amewaomba mashabiki wa Simba wamuombee msamaha kwa jamaa waliyowekeana naye ahadi ya kumpa mkewe endapo Yanga ikifungwa.

Jimmy akiongea na mbele ya waandishi wa habari, amesema kuwa aliahidi kumuweka rehani mke wake endapo Simba itashinda, na kwa matokeo ya jana Simba ilifanikiwa kushinda goli 1-0 jambo ambalo lilimfanya atimize ahadi ya kumuweka rehani.

Mimi nilisema hayo kwa sababu naipenda Yanga, najua timu yangu sio nzuri lakini sikupenda tuonekane wanyonge. Niliwekeana ahadi na shabiki wa simba anaitwa Kessy, kuwa endapo Simba itashinda nitampa mke wangu. Nawaomba msamaha, mnisamehe kwani timu yangu ni mbovu ila naipenda sana ndio maana nilifanya hivyo,“amesema jimmy.

Jimmy katika kipindi cha Kipenga Extra cha East Africa Radio, aliahidi kuwa endapo Yanga ikifungwa na Simba, atamweka rehani mkewe na yeye mwenyewe kuvua nguo Kariakoo.

Kwa upande mwingine msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amemuombea msamaha shabiki huyo kwa kusema “Ninakuombea msamaha ili mkeo anusurike!!Simba ni watu waungwana na kwa kuwa umeomba radhi tunaamini uliyepinga nae atakusamehe pia, Ila next time iwe fundisho kwa wafuasi wa Mbuteni msithubutu kutoa ahadi kwa Bingwa wa nchi,!!Naambiwa kuna wadada walisema wawe Mboga,sijui habari zao zipoje!!

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW