Michezo

Jamal Malinzi: Nitaendelea kuwa karibu na vijana wa ‘Serengeti Boys’

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba ataendelea kuwa karibu na vijana na Timu ya Tanzania ya vijana ‘Serengeti Boys’ licha ya kuondolewa na Congo kwenye harakati za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika Madagascar, hapo Aprili, mwakani.

????????????????????????????????????

Mipango ya TFF kwa sasa inayoongozwa na Malinzi kwa sasa ni kuiiingiza timu hiyo kwenye program ya timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 maarufu kwa jina la Ngorongoro Heroes baada ya kuguswa na kilio cha vijana hao ambao walishindwa kujizuia kumwaga machozi mbele ya Malinzi ambaye alifanya kazi kubwa kuwatuliza pamoja na viongozi wengine.

Serengeti Boys ilipoteza mchezo dhidi ya Congo Oktoba 2, 2016. Kwa kupoteza mchezo huo dakika ya pili kati ya nne ya nyongeza baada ya kumalizika kwa dakika 90, kumefanya vijana hao wa Tanzania kuenguliwa kwenye mashindano ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika – fainali zitakazofanyika Madagascar.

Dakika moja ndiyo iliyoipoteza Serengeti Boys kufuzu kwa fainali hizo kwa bao la dakika ya 92 la lililofungwa na Mountou Edoward.

“Niko nanyi, najua mna group la WhatsApp, naomba msifute namba yangu. Iwe humo na mambo yenu mengi naomba mniambie humo, na nitayashughulikia iwe binafsi au kiofisi. Nawahakikishia sitawaacha,” alisema Malinzi alipowafariji vijana hao ambao wameingia jana saa 3.00 usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege ya Rwanda.

“Umri wenu bado sana wa kucheza soka. Program za TFF, CAF na FIFA ziko nyingi pia mnaweza kupata nafasi ya kucheza Olimpiki na kuna michuano mingi, sitawaacha,” alisema Malinzi na kusisitiza ana imani na timu hiyo ambayo kwa dakika 90 za mchezo dhidi ya Congo walipambana kwelikweli kutetea taifa lao pendwa Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents