Michezo

Jamhuri Kihwelu Julio atangaza kuachana na kazi ya ukocha

Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelu Julio, ametangaza kujiuzulu kufundisha soka la nchini Tanzania kufuatia kutoridhishwa na maamuzi yanayofanywa na marefa.

makochaa

Uamuzi huo umeonekana kuwashtua wengi. Hiyo ni baada ya kupata kichapo kutoka kwa Mbeya City akiwa katika uwanja Sokoine Mbeya kwa kupoteza kwa goli 1-0.

Baada ya mechi hiyo aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa kwa sasa atakuwa anaenda kuangalia mpira uwanjani ila hawezi tena kuwa kocha wa mpira Tanzania.

“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwaajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana,” alisema.

“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano ya kimataifa havifanyi vizuri,” aliongeza.

“Kwahiyo kuanzia sasa hivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, nawawashuru watanzania wote waliokuwa karibu na Julio.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents