Shinda na SIM Account

Jamii yaaswa kuwajali watoto wenye mahitaji maalum

Tume ya Utumishi wa Walimu imetoa msaada wa Vyakula na Vinywaji kwa Kituo cha Kulea watoto wenye Utindio wa ubongo cha Miyuji Cheshire cha Mjini Dodoma.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Tume hiyo Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Bi Devotha Gabriel amesema kuwa msaada huo unajumuisha Unga, mchele, sukari, juice , mafuta ya kupikia, sabuni na vitenge kwa ajili ya walezi wa kituo hicho.

“Watoto wenye mtindio wa Ubongo ni watoto kama watoto wengine hivyo wazazi wasiwafiche watoto hao bali wawapeleke katika vituo maalum ili wafundishwe stadi mbalimbali za maisha,“ Alisisitiza Bi Devotha .

Akifafanua Bi. Devotha amesema kuwa Tume hiyo inaguswa sana na mahitaji ya watoto hasa wenye mahitaji maalum ndio maana katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani wameamua kuwaona watoto na kutoa zawadi kama wazazi na tunao wajibu wa kushiriki kikamilifu kuwalea watoto hawa.

Kwa upande wake Mtawa (Sister) Theresia Cosmas, ameshukuru Tume hiyo kwa kuona umuhimu wa kutoa msaada huo wa vyakula kwani utasaidia kwa kiwango kikubwa na unaonyesha moyo wa upendo kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.

Pia Alitoa wito kwa Taasisi nyingine za Serikali na Wadau mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono juhudi za tume hiyo kwa kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum wapatao 40 wanaolelewa katika Kituo hicho.

Tume ya Utumishi wa Walimu imekuwa moja ya Taasisi za Serikali zinazojitolea kushughulikia changamoto zinazokabili makundi maalum katika Jamii wakiwemo watoto.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW