Habari

Janet Jackson atajwa ‘rasmi’ kuwa bilionea, Forbes wabisha sio bilionea (Details)

Dada wa mfalme wa Pop marehemu Michael Jackson, Janet Jackson ametangazwa rasmi na jarida la Variety kwenye makala yake ya Janet Jackson: Beyond the Velvet Rope kuwa bilionea kutokana na kuwa utajiri wake binafsi unaozidi dola bilioni moja.

Janet-Jackson-900x1188-196kb-media-402-media-152295-1251556524

Kwa mujibu wa Variety, Janet mwenye miaka 47 ameweza kutengeneza dola milioni 458 zilizotokana na show za ziara alizofanya, dola milioni 304 zilizotokana na ushiriki wake katika movie ikiwemo ile ya Eddie Murphy ‘The Nutty Professor 2’ na zingine. Pesa zingine alizotengeneza ni dola milioni 268 kupitia mauzo ya albam na dola milioni 81 kutoka katokana deal za makampuni pamoja na udhamini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Janet amefanikiwa kuifikia status ya ubilionea ambayo haikuwahi kufikiwa na marehemu kaka yake king wa pop Michael Jackson pamoja na uwezo wote aliokuwa nao enzi za uhai wake, na ameingia katika orodha ya watu maarufu ambao ni mabilionea kama queen wa talk show Oprah Winfrey, legendary film director Steven Spielberg na wengine.

Upande wa pili mtandao wa Forbes umepingana na ripoti ya Janet Jackson kutajwa ‘rasmi’ kama bilionea kwa sababu kadhaa walizozitoa.

janet n hubby

Forbes wanasema habari ambazo zimetolewa hazisemi moja kwa moja kuwa Janet ni bilionea, zinaonesha tu kiasi cha pesa ambacho ameweza kutengeneza kutokana na kazi zake za burudani.

Kwa mujibu wa tafsiri waliyoitoa forbes ya mtu anaeweza kuifikia status ya ubilionea ni kuwa thamani ya pesa na mali zote anazokuwanazo mtu kwa wakati huo na sio kiasi gani cha pesa mtu kaingiza kutokana na kazi zake za kipindi chote toka aanze kazi.

Wakiendelea kuelezea jinsi ambavyo wao huwatathmini watu wa kuingia katika orodha yao ya watu mabilionea duniani, wamesema huangalia vitu kama umiliki wa hisa, mali zisizohamishika na mapato yatokanayo na kazi za sanaa.

Forbes walitoa mfano wa kwanini Oprah ni bilionea kwa kusema ni sababu ya umiliki wake wa hisa katika network ya Discovery na Harpo productions na sio kwasababu ya mapato yatokanayo na talk show yake ‘Oprah Winfrey Show’.

Waliendelea kusema hii si mara ya kwanza kwa habari za kupotosha kuhusu ubilionea wa watu maarufu, wakiongeza mfano wa Jessica Simpson aliwahi pia kutajwa kuwa bilionea bila kuzingatia vigezo walivyoviorodhesha na kutoa mfano wa Madonna kuwa ni tajiri lakini sio bilionea.

Janeth Jackson mwaka jana alifunga ndoa ya siri na bilionea wa kiarabu aitwaye Wissam Al Mana kutoka nchini Qatar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents