Burudani

Janet Jackson na Jermaine Dupri waanza kunyemeleana upya

Mwanamuziki Janet Jackson na aliyekuwa mpenzi wake miaka kadhaa iliyopita, Jermaine Dupri wanadaiwa kuwa na mawasiliano ya ukaribu uno hali inayo weza kufanya wakarejesha mahaba yao.

Haya yamebainishwa na mtu wa karibu wa wawili hao kupitia E! na kusema kuwa mrembo huyo aliyeachana na mumewe, Wissam Al Mana miezi kadhaa iliyopita amekuwa akiwasiliana na mno na producer Dupri na wamekuwa karibu sana hivyo usishangae wakirudisha mahusiano yao ya kimahaba kama ilivyokuwa awali.

Janet (51) na Jermaine, (45) walikuwa kwenye mahaba mazito kwa muda mrefu mpaka 2009 ambapo walimwagana.

Usemi wa waswahili ni kwamba mahawara hawaachani hivyo usishangae dada yake na Michael Jackson, Janeth akalea mtoto wake na Jermaine kwani hakuna linaloshindikanana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents