DStv Inogilee!

January Makamba azindua rasmi tuzo za ‘Under-30 Youth’ ashauri ziwatambue pia vijana wa mikoani

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Ndugu January Makamba, leo amezizindua rasmi tuzo za kwanza vijana walio chini ya miaka 30 (Under-30 Youth Awards) zinazotolewa na taasisi ya Youth For Africa (YOA).

January Makamba  akizundua rasmi tuzo (800x533)
January Makamba akizundua rasmi tuzo

Mkurugenzi Mkuu wa YOA, Awadh Milasi (800x533)
Mkurugenzi Mkuu wa YOA, Awadh Milasi

Uzinduzi wa tuzo hizo umefanyika kwenye kituo cha ubunifu wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Masiliano, ICT cha Kinu kilichopo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya vijana waliotajwa kuwania tuzo hizo, wadhamini na wadau wengine muhimu.

Awadh (533x800)

Catherine Barreto - KINU (533x800)

Fredrick Bundala, Bongo5 akikabidhi tshirt (800x533)
Fredrick Bundala, Bongo5 akikabidhi tshirt

Gavin Gosbert mwenye koti (800x533)
Mmoja wa vijana wanaowania tuzo hizo, Gavin Gosbert mwenye koti

IMG_7152 (800x533)

IMG_7162 (800x533)

Licha ya kufanya uzinduzi huo, Ndugu Makamba pia ametoa vyeti kwa vijana waliotajwa kwenye tuzo hizo.

IMG_7219 (800x533)

IMG_7221 (800x533)

IMG_7223 (800x533)

IMG_7228 (800x533)

IMG_7230 (800x533)

IMG_7238 (800x533)

IMG_7241 (800x533)

IMG_7244 (800x533)

IMG_7246 (800x533)

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutoa vyeti hivyo, Makamba ameipongeza taasisi ya YOA kwa kuanzisha tuzo hizo kwakuwa zitawapa moyo vijana ili waendelea kujituma zaidi. Aidha amewashauri waandaji kuzitanua zaidi tuzo hizo ili ziwatambue pia vijana waliopo kwenye mikoa mingine nchini.

“Hili ni jambo jema tunaliunga mkono na tunadhani kwamba lisiishie Dar es Salaam peke yake, wapo vijana wengi kwenye mikoa yote Tanzania ambao wanatoa mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya jamii yetu katika Nyanja mbalimbali na wenyewe lazima watambulike, lazima tuwatuze na kuwatia moyo,” alisema.

Akizungumzia kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana nchini, January ametoa wito kwa vijana kujituma na kutokata tamaa na kuzingatia suala la nidhamu.

“Wakati mwingine sio kile ulichosemea ung’ang’anie ufanye hicho hicho tu, wapo vijana wengi ambao wamesomea kitu kimoja, wametafuta na kuona fursa kwenye mambo mengi na wenyewe wamefanya.”

Akielezea kuhusu vigezo vilivyotumika kuyapata majina ya wanaowania tuzo hizo naye Mkurugenzi Mkuu wa YOA, Awadh Milasi amesema majina hayo yamepatikana kwa njia ya wazi na halali.

“Tumejaribu kutengeneza grounds of fairness. Tukizungumzia umri unategemea hawa vijana ambao wapo shule ya sekondari, chuo au wamemaliza chuo au ndio kwanza wameingia kazini. Lakini vile vile hatuangalii rangi, dini, kabila kikubwa ni ule mchango waliofanya,”alisema.

January Makamba (533x800)
January Makamba

January Makamba kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa YOA (800x533)
January Makamba kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa YOA

MC (533x800)
MC

Michael Mbwambo (800x533)
Michael Mbwambo, Popote Media

Nsia Swai, Onspot Magazine (533x800)
Nsia Swai, Onspot Magazine

Osse Sinare na Pedaiah Swank (800x533)
Osse Sinare na Pedaiah Swank

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na  wadhamini wa tuzo hizo (800x533)
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wadhamini wa tuzo hizo

Picha ya pamoja ya waliotajwa kwenye tuzo hizo (800x533)height=”533″ class=”aligncenter size-full wp-image-48505″ />
Picha ya pamoja ya vijana waliotajwa kwenye tuzo hizo

Rebeca Gyumi (533x800)

Wageni waalikwa (800x533)

IMG_7163 (800x533)

IMG_7166 (800x533)

IMG_7173 (533x800)

IMG_7183 (533x800)

IMG_7262 (800x533)

IMG_7263 (800x533)

IMG_7267 (533x800)

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa August 17.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW