Michezo

Januzaj aenda Sunderland kwa mkopo kutoka Man Utd

Mchezaji wa kimataifa kutoka Ubeligiji na Manchester United Adnan Januzaj, amejiunga na sunderland kwa mkopo msimu huu wa 2016/17.

_90776448_d1a11821-bd31-4831-9db7-e994068bc4af

Uhamisho huo umemuunganisha na meneja wake wa zamani David Moyes pamoja na wachezaji weza Donald Love na Paddy McNair aliyejiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 5.5 wiki hii.

Januzaj, alikuwa anataka kutoka Old Trafford kabisa lakini klabu hiyo ya United iliamua kumkabidhi kwa klabu hiyo kwa mkopo.

Amesha ifungia mabao matano katika mechi 63 alizoshiriki kwenye klabu ya United.
Mkataba wake na Manchester United utamalika mwaka 2018.

Winga huyo alijiunga na timu ya Borussia Dortmund msimu uliopita kwa mkopo wa miezi minne, lakini alishiriki katika mechi 12 kabla ya kurudi katika timu yake ya Manchester United.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents