Habari

Japan kuboresha miundombinu Dar

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Ichiro Aisawa baada ya kuona changamoto ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam amebaini kuwa nchi yake bado inahitaji kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha miundombinu ya Jiji hilo na kuahidi kufikisha ujumbe huo kwa Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Shinzo Abe.

Akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana ambapo walikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Ichiro ambaye aliahidi kufikisha ujumbe huo Japan.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Ichiro Aisawa kwa kuja Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa ambao Japan inautoa katika maendeleo, na itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Japan katika masuala mbalimbali.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents