Habari

Jason Derulo kuperform nchini Rwanda July 28


Mwanamuziki wa R&B wa nchini Marekani Jason Derulo anatarajiwa kwenda kutumbuiza mjini Kigali, Rwanda kwenye fainali za mashindano ya Primus Guma Guma Superstar Season 2 (PGGSS 2) July 28, 2012.
Primus Guma Guma SuperStar ni shindano la muziki nchini Rwanda ambalo huwaleta wasanii wote wakubwa kushindana na mshindi kupewa jina la Primus Guma Guma SuperStar.
Shindalo la kwanza lililofanyika mwaka 2011 mshindi alikuwa ni mwanamuziki wa R&B nchini humo Tom Close.
Upekee wa shindano hili ukilinganisha na mashindano kama BSS na Tusker Project Fame, ni kwamba lenyewe hushindanisha wasanii waliofanikiwa tayari (masupastaa) na wasanii kumi pekee ndio huchaguliwa kushiriki.
Wasanii hao hutumia nyimbo zao wenyewe wakati wa shindano hilo.
Vigezo vya wanamuziki kushindana kwenye shindano hilo ni lazima awe na miaka 18 na kuendelea, awe na wimbo uliohit na awe anafanyia muziki nchini Rwanda.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents