Burudani

Jay Moe adai hawezi kufanya kazi na msanii wa nje wakati hana video za kutosha

Rapper Jay Moe amefunguka kuwa hawezi kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka nje wakati bado hana video nyingi nzuri ambazo zitaweza kumshawishi kufanya naye kazi.

Moe amekiambia kipindi cha On The Eight cha TVE kuwa hawezi kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka nje mapaka atakapokuwa na video walau tano ambazo msanii huyo ataweza kuziangalia na kuufahamu uwezo wake zaidi tofauti na ilivyokuwa sasa bado hana video za kutosha.

Hitmaker huyo wa Pesa Madafu ameongeza hata alipokuwa Afrika Kusini mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini P-Funk Majani alimpigia simu na kumtaka kushoot video huko lakini alimwambia kuwa yupo huko kwa ajili ya kushoot video moja ya kutimiza miaka yake 11 bila ya kuwa na video nyingine.

Jay amesisitiza kuwa akifikisha video za kutosha itakuwa ni vizuri kwake hata zikichezwa kwenye vituo vingine vikubwa vya nje ya nchi ikiwemo Nigeria. Rapper huyo kwa sasa ameachia video yake mpya ‘Nisaidie Kushare’ baada ya wimbo wake wa ‘Pesa Madafu’ kufanya vizuri kwenye redio na runinga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents