Habari

Jay Moe anakuja na Mocumentary

Jay MoeMpaka sasa Jay Moe ameshatoka na mkono ambao umekuwa ni gumzo jijini ujulikanao kwa jina la ‘hadithi tatu tofauti’ akiwa ameufanyia katika studio za Kama kawa Records, na si hayo tu

Jay Moe


Mpaka sasa Jay Moe ameshatoka na mkono ambao umekuwa ni gumzo jijini ujulikanao kwa jina la ‘hadithi tatu tofauti’ akiwa ameufanyia katika studio za Kama kawa Records, na si hayo tu mchizi amejipanga kikamilifu kwani anatarajia kuikamilisha albam hiyo ikiwa inaambatana na DVD ambayo itakuwa ikielezea historia ya maisha yake katika sanaa.


“nimekuwa kimya kwa muda mrefu sana kiasi kwamba mashabiki wangu wamekuwa wana hamu na ujio wangu, nachopenda kusema ni kuwa wimbo wa ‘hadithi tatu tofauti’ nimeutoa lakini sioni kama nimetoa hit kwani mikono ambayo nimeshaifanya ni noma na sijawahi kusikika hivi na navyokuja kwa jinsi ambavyo nimejipanga sasa”


alielezea jinsi malengo yake ya kuama kuiita albam yake Mocumentary “unajua watu wanapenda tu kuja na majina ambayo hayaambatani na kile kilichomo ndanoi ya Albam ndio maana mimi nimeamua kufanya hivi kwani hii si albam ila ni documentary ya maisha yangu toka nilipoanza muziki na mpaka nilipofikia na kuelezea kila aliyeshiriki katika kuifanikisha sanaa yangua na kuniangusha katika gemu.


Mpaka sasa albam imeshakamilika na Moe yukoa mbioni kukamilisha DVD yake ya Mocumentary.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents