Burudani

Jay Moe awacharukia wanaotaka kumgombanisha na WCB

By  | 

Msanii mkongwe wa muziki hip hop Bongo, Jay Moe amezitaka kurasa za mitandao ya kijamii kuacha kuandika habari za uongo.

Mapema leo msanii huyo ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwataka wanaoendesha page hizo kuacha tabia ya kucopy na kupaste habari bila kuwa na uhakika.

“To @udakutz_ naheshimu sana kazi ka mikono yenu, sijawahi kufanya Interview na nyie wala kunicontact for an interview…tafadhali naomba muache kucopy na kupaste vitu namna hii, I have huge respect [email protected] n #WASAFI kwa ujumla, tufanye vitu vya kujenga sio kubomoa,” ameandika Jay Moe

Aliongeza msanii huyo wa ngoma ya Nishaidie Kushare “Sina Tatizo Na kupeleka nyimbo zangu #wasafidotcom na hakuna sehemu nimesema sitopeleka so Dont Get It Twisted, kusema sitosign its because I have my own label #SoFamous, so Please next time kama mnahitaji udaku kama huu msisite kinitafuta lakini sio kufabricate story @udakutz_ kwa niaba ya #SoFamous napenda kusema kwamba hii ni wrong Info..#Nisaidie_Kushare???

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments