Burudani

Jay Moe kuachia ngoma 2 ‘CBM’ ft AY, Cpwaa & Mr Blue na ‘Only U’ ft. Ommy Dimpoz

Mtoto wa Mchopanga, Jay Moe anatarajia kuvunja ukimya wake kwa kishindo atakapoachia ngoma mbili ukiwemo ‘CMB’ aka Check Bob Maarifa aliowashirikisha AY, Cpwaa na Mr Blue.

page

Wa pili ni Only You aliomshirikisha Ommy Dimpoz.

“Soon tunaweza tukarelease ngoma mbili kuna ambayo nimefanya na Ommy Dimpoz “Only you” na nyingine nimemshirikisha AY,Cpwaa na Mr Blue ambayo Cpwaa amefanya chorus na Mr Blue na AY wamefanya verse hiyo nyimbo inaitwa CBM,” Jay Moe ameiambia Bongo5.

“Zamani nilifanya muziki kama bishoo sasa hivi tena siyo bishoo ni CBM kwasababu enzi zile unafanya ubishoo halafu hauna maarifa yoyote unategemea maisha ya home, unaazima nguo kwa masela ili upendeze kwahiyo najaribu kuwabadilisha watu wengine kwamba unaweza ukawa Check Bob halafu ukawa na maarifa yako na pia nimemshirikisha AY kwasababu AY alikuwa kwenye CBM crew miaka hiyo kabla hajatoka kuwa AY huyu na nimemshirikisha Mr Blue kwasababu kila mtu anamjua Mr Blue ni Check Bob.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents