Habari

Jay Z aingia katika biashara ya ‘Perfume’, kuzindua perfume zake za ‘GOLD’ mwezi huu

Rapper na mfanyabiashara Sean Carter aka Jay Z ni mjasiriamali ambaye anaendelea kujitengenezea pesa nyingi kupitia miradi mbalimbali aliyonayo, na sasa anaongeza biashara nyingine mpya ya perfume zake za kiume ‘GOLD’.

Jay z n bey

Mwaka huu Jay Z alikamata nafasi ya pili katika orodha ya jarida la Forbes ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza mkwanja zaidi ‘Hip Hop Cash Kings 2013’ kwa kuingiza dola milioni 43 kupitia michongo mbalimbali ikiwemo muziki, biashara anazomiliki na sasa anaongeza perfume zake zinazoitwa ‘GOLD’ ambazo huenda zitamuongezea pato lake la mwaka.

gold-jay

Perfume za ‘Gold’ zinatarajiwa kuzinduliwa November 20, na bei zake zitakuwa kati ya $39 hadi $70. Gold zitapatikana katika chupa tatu zenye ujazo tofauti. Pia kuna mpango wa kuongeza deodorant pamoja na shower gel zitakazosindikiza perfume hizo.

Source: Global Grind

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents