Burudani

Jay Z apanda kizimbani kutoa ushahidi wa kesi ya haki miliki ya hit yake ‘Big Pimpin’

Jay Z ameamua kuwa mpole na kukubali kuingia mahakamani kutoa ushahidi jijini Los Angeles, Jumatano hii kwenye kesi inayomkabili ya kukiuka masuala ya haki miliki kufuatia wimbo wake wa mwaka 1999, Big Pimpin.

Jay Z ameiambia mahamakama kuwa haamini kama alivunja sheria za haki miliki katika matumuzi ya kionjo cha wimbo wa kiarabu kutengeneza wimbo huo uliohit.

Jay Z ambaye jina lake halisi ni Sean Carter na Timbaland, aliyetayarisha wimbo huo walidaiwa kutumia vionjo kutoka kwenye wimbo wa Baligh Hamdi wa Misri wa mwaka 1957, Khosara Khosara bila ruhusa.

https://www.youtube.com/watch?v=BQmfDaSc7E8

Rapper huyo alitumia dakika 90 kutoa ushahidi kwenye mahakama ya Los Angeles ambako alitoa pia historia ya maisha yake, mafanikio na mchakato wa kiubinifu yeye na Timbaland walitumia kutengeneza wimbo huo.

“We have the rights as you can see on the bottom of the CD,” aliiambia mahakama kumaanisha kuwa walitoa credits kwa Khosara Khosara.

Timbaland naye alikuwepo mahakamani hapo kutoa ushahidi.

Wanasheria wa Jay Z na Timbaland wanadai kuwa wawili hao wameshalipia gharama za sample hiyo. Kesi hiyo imerejea tena baada ya miaka minane.

Binamu yake na Hamdi, Osama Ahmed Fahmy aliwasilisha mashtaka mara ya kwanza mwaka 2007. Hamdi na muimbaji wa wimbo huo, Abdel Halim Hafez, wote wamefariki.

Mwanasheria wa Timbaland, Christine Lepera alisema mtayarishaji huyo alitumia vionjo vya wimbo huo kwa kudhani ni wimbo huru lakini walikuja kulipa $100,000 kwa EMI Music Arabia kupata kibali.

Mwanasheria wa Fahmy, Peter Ross alidai kwa wawili hao walitakiwa pia kuomba ruhusa kutoka kwa familia pia lakini kwa makusudi walikwepa kwkuwa walijua wasingepewa kutokana na mashairi ya Big Pimpin kuwa machafu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents