Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Jay Z ambwaga Diddy kwenye orodha ya matajiri wa Hip Hop duniani

By  | 

Jay Z ameonyesha ukubwa wake kwa mkwanja wake anaomiliki. Forbes imemtaja rapper huyo kuwa na utajiri wa dola milioni 900 na kumfanya kumbwa P Didy ambaye amekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa miaka takriban saba.

Rapper huyo ameingiza fedha hizo kutokana na biashara zake nyingi ikiwemo Tidal, mauzo ya Album, ziara zake za muziki, lebo yake ya Roc Nation, Roc Nation Sports, na vinywaji vya Armand De Brignac na D’Usse Cognac.

Wakati huo huo Diddy anashika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa dola milioni 825 ikiwa ni ongeeko la kiasi cha dola tano kutokana na utajiri wake wa mwaka jana uliotajwa kuwa ni dola milioni 820 ambao ulimfanya kuongoza katika orodha hiyo.

Wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni Dr. Dre ($770) milioni, Drake na Eminem wenye ($100) milioni. Kwa mwaka jana orodha hiyo iliongozwa na Diddy akifuatiwa na Jay Z, Dr. Dre, Birdman na Drake.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW