Jay Z amfagilia Obama

Nyota wa Muziki wa Hip hop duniani Jigga Jay Z hivi karibuni alifanya bonge la Show jijini New York, lakini kali kuliko zote ni pale Jigga aliposikika hadharani akiongea maneno yaliyowapa picha mashabiki kuwa anamfagilia bwana Barack Obama



Jay Z


 


Nyota wa Muziki wa Hip hop duniani Jigga ‘Sean Carter’ Jay Z hivi karibuni alifanya bonge la Show jijini New York akiwa na mshikaji wake Mary J Blige, inasemekana kwamba kila aliyehudhuria alionekana kuvutuiwa na kumuona akiwa sambamba na Blige jukwaani.



Lakini kali kuliko zote ni pale Jigga aliposikika hadharani akiongea maneno yaliyowapa picha mashabiki waliokuwepo katika onesho hilo kuwa anamfagilia mgombea wa kiti cha uraisi wa Marekani bwana Barack Obama na kumdisi live Raisi wan chi hiyo mheshimiwa George W. Bush.



Jigga alisikika akiwauliza mashabiki waliokuwemo katika ukumbi huku akirudia mara kwa mara “mko tayari kwa mabadiliko” pia aliweka wazi na kutaka ieleweke kuwa onesho hilo halihusiani na kudhaminiwa na mgombea huyo wa kiti cha uraisi Bwana Barack Obama kwa ajili ya kampeni.



Minong’ono ya utani ilisikika ikisema kuwa iwapo Obama atashinda katika kinyang’anyiro hicho upo uwezekano kwa Jay Z akakosa cha kurap.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents