Burudani

JAY Z Atua Manchester kwa Helicopter


Akiwa miongoni mwa wasanii wa hip-hop waliofanikiwa zaidi, si jambo la kushangaza Jay-Z akiamua kusafiri kwa style na kuachana na ndege. Nguli huyo jana aliwasili mjini Manchester, Uingereza kwa helicopter kwajili ya show ya ‘Watch The Throne’.
Jay-Z alionekana kusafiri peke yake akisindikizwa na bodyguard aliyekuwa makini kumlinda wakati anashuka kuingia kwenye uwanja wa Etihad wa Manchester.

Hata hivyo kundi la mashabiki halikusita kuisogolea helicopter hiyo ya rangi nyekundu kumuona kwa ukaribu Jigga.
Wakati mabodyguard wake wakiwa tayari kumwongoza kwenye gari, Jay aliwaambia anafurahia kusaini autographs na kupiga picha na mashabiki wake.
Jay alikaa kwa muda na kupiga story mbili tatu na mashabiki wake waliokuwa na furaha kubwa kuongea naye kabla ya kuingia kwenye kitu cha limousine.
Inapendeza kuona kuwa jamaa bado ni mnyenyekevu na hana pozi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents