Burudani

Jay Z kuachia albamu mpya?

Ni kweli Jay Z anataka kuachia albamu yake mpya sasa hivi? Hilo ndio swali ambalo mashabiki wengi wanajiulisa katika vichwa vyao.

Ni miaka takriban minne imepita tangu rapper huyo alipoachia albamu ake ya mwisho ‘Magna Carta… Holy Grail’ mwaka 2013. Mabango yaliyoandikwa 4:44 ndio yaliyowachangana mashabiki ambapo yameonekana kuwepo katika sehemu kubwa ya jiji la New York na Los Angeles, Marekani ambayo ndio yaliyozua tetesi za ujio mpya wa albamu hiyo ya Jay Z.

Hatua hiyo imewafanya mashabiki kukumbuka ujumbe wa Swizz Beatz, aliouandika mwezi uliopita katika mtandao wa Instagram, ikimuonyesha yupo na Jigga na kuandika, “Album ModeZone.”

Hata hivyo namba nne imekuwa na mahusano makubwa katika familia ya Carter, ambapo Jay mwenyewe amezaliwa Disemba 4 huku mkewe Beyonce akizaliwa Septemba 4. Mwaka 2011 Queen Bey aliachia albamu iitwayo ‘4’ na hata jina la katikati la mtoto wao Blue Ivy linamaana ya namba 4 kwa lugha ya kirumi.

Wakati huo huo Jay Z alichora tattoo ya 4 katika vidole vyake vya mkononi wakati wa harusi yao. Swali ni kweli rapper huyo ataweza kuachia albamu hiyo kukata kiu za mashabiki wake kama tetesi hizo zilivyosambaa?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents