Burudani

JAY Z sasa anataka jina lake liandikwe bila kuwekewa alama (-) ‘JAY-Z’

Kama wewe ni kati ya watu ambao huwa wanaliandika jina ja Baba Blue Ivy kwa namna tofauti, sasa Hova ametoa maelekezo ya jinsi anavyotaka jina lake la jukwaani liandikwe.

Jay Z jina2

Shawn Carter baba wa mtoto mmoja ‘Blue Ivy’ na mume wa mwanamuziki mrembo Beyonce ametoa maelekezo kwa wachapishaji wa majarida na waandishi kwa ujumla kuwa sasa jina lake la jukwaani liandikwe JAY Z, alichokiondoa ni alama (-) kati ya Jay na Z, ambayo ilikuwa zamani ikiandikwa ‘JAY-Z’.

Jay Z kupitia label yake ya Roc Nation amewatumia ujumbe wa mabadiliko hayo wachapishaji mbalimbali na waandishi ili wasitumie tena ‘punctuation mark’ (-) katika jina lake. Hii si mara ya kwanza kwa Jay Z kutaka kuiondoa alama hiyo katika jina lake japo mara ya kwanza inaonekana hakuitilia maanani sana.

Mabadiliko hayo yameanza kuonekana hata katika artwork ya album yake mpya ya Magna Carta Holy Grail jina lake limeandikwa bila alama hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents