Siasa

Jaydee asifiwa kuvaa mavazi ya heshima

Lady JayDeeBAADHI ya wananchi wamepongeza mabadiliko ya mavazi aliyonayo mwanamuziki Judith Wambura, maarufu kama Lady Jaydee.

Lady Jaydeena Irene Mark


BAADHI ya wananchi wamepongeza mabadiliko ya mavazi aliyonayo mwanamuziki Judith Wambura, maarufu kama Lady Jaydee.


Pongezi hizo zilitolewa juzi na watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mashuhuri akiwamo Rais Jakaya Kikwete.


Akiwa ukumbini hapo, Jaydee alionekana kuvalia nguo za heshima kiasi cha kubadili muonekano wake wa siku zote. Alikuwa na bendi yake ambapo kwa mara kadhaa waliwatumbuiza waalikwa.


“Tumezoea kumwona nusu uchi, tofauti na leo…hii ni dalili kuwa amekua na ameamua kubadili mwonekano wake kuanzia kwenye mavazi, kweli kama kukua sasa amekua na anapendeza,” alisema mmoja wa waalikwa waliokuwa meza moja na mwandishi wa habari hizi.


Naye Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za binadamu, Hellen Kijo-Bisimba, aliunga mkono kauli hiyo kwa maelezo kuwa nguo za heshima zinampendeza mwanamuziki huyo na kuzoa watazamaji wa rika zote.


“Anapovaa kiheshima ananishawishi hata mimi kumtizama…ukweli navutiwa na nyimbo zake na kama ameamua kuvaa kwa heshima kama leo, basi ni hatua nzuri sana,” alisema Kijo-Bisimba.


Mwanamuziki huyo anayetamba na kibao cha ‘siku hazigandi’ alivaa sketi pana ya ngazi tatu iliyofika chini ya magoti na blauzi nyeusi ya mikono mirefu iliyofunika tumbo na ndani alivaaa ‘top’ nyeusi.


Souce: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents