Jaza Fomu ya Shindano la Mama Shujaa wa chakula hapa!

1006258_630924213586534_220399988_a

“GROW. Food. Women. Planet.” ni kampeni iliyoanza mwaka 2011 na inatarajiwa kumalizika mwaka 2015. Kampeni hii inalenga kuhakikisha kuwa kila mtu ana chakula cha kutosha kila siku “everyone has enough to eat always”.

Kampeni inasisitiza upatikanaji wa chakula ambacho kinahitajika na kinakidhi ukuaji wa afya, akili, maisha na dunia.

Kampeni ya Grow inaamini chakula ni sehemu ya tamaduni, afya, na ni stahiki ya kila mmoja wetu.

Grow si kampeni ya kutoa misaada ya chakula, ila ni kampeni ya kuhakikisha dunia inazalisha, inasambaza, inahifadhi na inatumia chakula inavyostahili. Kwa kifupi, kampeni ya Grow inataka kubadilishwa kwa mfumo mzima wa chakula duniani kwani chakula ni HAKI YA MSINGI ya kila binadamu. Haki ya kuishi haipatikani kama Haki ya kupata uhakika wa chakula haitekelezwi.

Fuata link hii, kujaza fomu ya shindano la Mama Shujaa wa chakula, na upate nafasi ya ushindi!

Bonyeza Hapa kujaza Fomu

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW