Burudani

JB akiri kuwa bongo movie imesinzia

Msanii wa industry ya movie hapa bongo, Jacob Stephen maarufu kama JB, amesema movie zimesinzia kwa sasa na kwamba zinatakiwa kupelekwa level nyingine ya juu zaidi.

Jacob Stephen aka JB akisoma mshindi

Akizungumza na 255 ya XXL inayoruka kupitia Clouds FM, JB amesema, “Kiukweli bongo movie imesinzia kwa sasa lakini haijafa kama watu wengine wanavyosema kinachotakiwa kufanyika ni kuinua movie zetu na kuzipeleka level nyingine ya juu itasaidia kuboost na kurudisha heshima ya movie hapa bongo.”

“Hata muziki nao mwanzo ulionekana kusinzia kabla ya wasanii wenyewe kwenda nje na kuanza kufanya video kali za nyimbo zao mpaka sasa wanaonekana kufanya vizuri,” aliongezea JB.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents