Technology

Je, IGTV inalipa kama YouTube? fahamu mfumo huo mpya wa Instagram unaoruhusu mtumiaji ku-upload video ndefu hadi dakika 60

Jana Juni 20, 2018 Bongo5 mtandao wa Instagram ulizindua rasmi huduma yao ya IGTV ambayo itamuwezesha mtuamiaji kuweka video ndefu kwenye mtandao huo pendwa duniani.

IGTV ni nini?

Hii ni feature mpya iliyozinduliwa na mtandao wa Instagram siku ya jana ambayo itakuwezesha mtumiaji ku-upload video ndefu za kuanzia sekunde 15 hadi dakika 60.

IGTV inapatikana wapi na video za aina gani zinaruhusiwa kuwekwa?

Kwa sasa feature (sehemu) hii mpya inapatikana kwenye App ya Instagram ya kawaida sehemu ya juu ya Insta  Story.

Au unaweza ukapakua App ya IGTV moja kwa moja kutoka Play Store kwa watumiaji  wa Android na App Store kwa watumiaji wa iOS .

Na je, ni video gani zinazotakiwa kupandishwa kwenye IGTV?

Hapa kidogo kuna vigezo vingi vya aina ya video zinazotakiwa kupandishwa kwenye IGTV ukilinganisha na mitandao mingine kama YouTube n.k . na vigezo ni (i). Lazima video iwe  wima (vertical) na iwe kwenye mfumo wa MP4 (ii). Iwe angalau na Aspect Ratio  kati ya 4:6 hadi 9:16 . (iii) Video yoyote ile itakayopandishwa inatakiwa isizidi  GB 5.4.

NB: Instagram wameruhusu pia kupandisha video zenye ubora wa 4K ila endap video yako itaenda kinyume na masharti yao wataishusha wenyewe.

Vipi kuhusu malipo kupitia video utakazozipandisha?

Najua hapa watu wengi ndio wanapopahitaji kwani kila mtu anahitaji kutengeza mkwanja kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia mkutano wa uzinduzi wa IGTV uliofanyika jana mjini California, Instagram wamesema kuwa kwa muda huu hawataweka matangazo ila wanafikiria ndani ya miezi 12 ijayo kuanza kuruhusu matangazo ili kuanza kulipa watu wanaoweka video zao kwenye mtandao huo pendwa wa Instagram.

Unaweza ukajiuliza pia kwanini kuna App ya IGTV na ile hali App ya Instagram kuna sehemu IGTV inapatikana?

Ukweli ni kwamba Instagram wenyewe bado hawajaweka wazi kwanini wamefanya hivyo ila ninachokiona ni kwamba ukitumia App ya IGTV ni rahisi zaidi kupandisha video kuliko ukitumia IGTV iliyopo kwenye App ya Instagram.

Je, utafunguaje chaneli yako ya IGTV?

Nenda kwenye Icon ya IGTV kwenye ukurasa wako wa Instagram Bofya na link itakupeleka moja kwa moja kwenye IGTV na hapo itakuonesha alama ya + utachagua Create my Channel na utakuwa umekamilisha hatua za kufungua channel yako. Tazama video hapa chini kujua maelezo mengine ya jinsi ya kufungua channel

https://youtu.be/0yQ5Is3CiLU

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents