Michezo

Je Kylian Mbappe kutua Manchester United ?, aomba kuondoka PSG

Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameomba kuondoka ndani ya timu hiyo ifikapo mwakani 2021.

Mbappe mwenye umri wa miaka 21 amehusihwa kuelekea katika miamba ya soka England klabu za Manchester United na Liverpool.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha The Times, mkataba wa kinda huyo raia wa Ufaransa ndani ya PSG utafikia tamati ifikapo Juni 30, 2022.

Kinda huyo hatari zaidi mwaka 2018, alitangazwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi ambaye amefanikiwa kufunga goli katika michuano ya fainali ya kombe la dunia na kufanikiwa kuvunja rekodi ya Gwiji la soka duniani Pele na tangu wakati huo amekuwa miongoni mwa wachezaji ghali kunako ramani ya soka. Ameshafunga jumla ya magoli 90 katika michezo 124 aliyocheza PSG akiwa na 51 assists.

Liverpool ni moja ya klabu kubwa na yenye mafanikio katika michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya na yenye kocha bora kabisa.

Manchester United fans react to Marcus Rashford and Kylian Mbappe  comparison - Manchester Evening News

“Kile ambacho Liverpool inafanya katika kipindi hiki inavutia,” moja kati ya kauli za Mbappe ambazo amewahi kusikika akisema mwanzo kabisa mwa mwaka huu.

Mbappe ameongeza ”Unapowatazama unaweza kufikiria kilakitu kipo rahisi, lakini sio rahisi hivyo. Hawa watu wapo makini, wanacheza mechi kila baada ya siku tatu na wanachinda,wanashinda.

Wakati kuna kila dalili kuwa Manchester United ile ya zama za Sir Alex Ferguson inarejea hii ni baada ya kusajiliwa nyota kama Bruno Fernandes ambapo sasa, Ole Gunnar Solskjaer akiongoza jahazi hilo.

Mbappe ananafasi kubwa yakucheza akiwa United kuliko Anfield kwa kuwa kule kikosi kimekamilika pale mbele ambapo kuna Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firmino.

Kama United itakuwa na msimu mzuri na kufuzu kunako Champions League na kushinda baadhi ya vikombe basi itakuwa rahisi kwa kikosi cha Solskjaer kuwa na Mbappe pale mbele akishirikiana na Marcus Rashford na Anthony Martial.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents