Habari

Je na wewe hujitambui? Kwanini unatakiwa kujitambua?

Kujitambua ni uwezo na uelewa wa kujua wewe ni nani, una kusudi gani, wapi na watu gani kwa muda upi. Ni uwezo wa kujua wapi ulikotoka na wapi unaelekea na unatakiwa uwe kwenye eneo gani. Je unajitambua?

woman-thinking

Asili yako ni nini?

Katika harakati za kujitambua unaanzia kwenye asili yako, asili yako ni utu wako, kusudi lako na mpango mzima wa maisha yako. Kama umeelewa asili yako vizuri ni rahisi kujua wewe unapaswa kufanya nini wapi na watu gani, ingawa tumekuwa na tatizo la kutokujua wapi tunatoka na tuelewe wapi tunakwenda na watu gani? Bila kujua tumepoteza mwelekeo wa kile ambacho tunapaswa kufanya kila siku kufikia kule tunanatakiwa kufika katika maisha yetu.

Je Utu wako ni nini na unajengwa na nini?
Vijana wengi tumejikuta tukipoteza dira na maisha wakati mwingine kwa sababu utu wetu tumewauzia watu wengine kwa kubadilishana na fedha au umaarufu. Baada ya kuuza utu wetu tumelazimika kufanya mambo ambayo yatamfurahisha mtu fulani au au watu fulani lakini wakati huo huo tukiharibikiwa na hatuna mipaka ya namna tunavyoishi. Tumeingia kwenye mkumbo kwa kuwa hatujui utu wetu umejengwa na nini? Je ni fedha, maadili ya dini, umaarufu au marafiki zetu?

Je kila unachokifanya kila siku kinaleta msukumo kutoka wapi na kwa kusudi gani?

Msingi wa hicho unachofanya uko wapi?
Haya ni mambo ambayo hatutafundishwa shule au vyuoni unatakiwa utafute sehemu nyingine. Ukijifanya ni kipofu na ni upuuzi kuna siku vitu vinakutokea puani na hujui unaanzia wapi kutatua tatizo. Je malengo ya maisha yako unayatambua au unaendeshwa na malengo ya watu wengine? Msingi wako uko wapi?

Kujitambua ni mwanzo wa wewe kuweza kufikia malengo na kutokuingilia maisha kwa pupa au kufuata mkumbo. Roma haikujengwa kwa siku moja, hivyo hata maisha tunayoyatafuta hayatajengwa kwa siku moja ukienda kwa pupa lazima utapotea bila watu kujua. Tafakari na chukua hatua!

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents