Aisee DSTV!
SwahiliFix

Je, ni kweli Harmonize amefunga ndoa na mchumba wake Sarah?, Hakuna msanii hata mmoja kutoka WCB aliyehudhuria kwenye harusi (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize na mchumba wake Sarah kwa siku ya jana na leo wameendelea kugonga vichwa vya habari hapa Tanzania kwa tukio lao la kufunga ndoa.

Swali ni kwamba ni kweli wawili hao wamefunga ndoa? Au kuna kitu kingine kinaendelea.

Kwa mujibu wa marafiki wa karibu wa Harmonize wanaopenda zaidi kuweka vitu kwenye mitandao ya kijami, Wamesema kuwa wawili hao jana usiku wamefunga ndoa na ilihudhuriwa na watu wake wa karibu tu ambao anafanya nao kazi kwa sasa.

Bongo5 imemtafuta harmonize kuthibitisha taarifa hizo, Lakini namba yake haijapatikana licha ya video nyingi kusambaa mitandaoni zikionesha tukio la inayoonekana kama sherehe za harusi hiyo.

Hata hivyo, Mmoja ya watu wake wa uongozi wake kwasasa, Ambaye amekataa kutajwa jina, Amesema tukio hilo sio harusi kama inavyodhaniwa bali alikuwa location kwa ajili ya ku-shoot video yake mpya ijayo.

Wimbo huo bado haijajulikana lakini huenda ukawa ni ule wa ‘TUWAKOMESHE’ aliomshirikisha Lady Jaydee, Japokuwa bado kuna ukakasi kwani hata Lady Jaydee mwenyewe amempongeza harmonize kwa kufunga ndoa na hakuwepo kwenye tukio.

Mwananmitindo maarufu hapa Tanzania, Mustafa Hassanali alikuwa ndio mtu wa kwanza kuposti video ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika, “Hongera sana Sarah kupata Dume. Mungu abarike Ndoa ya Sarah na Rajabu ameen.“.

Kingine, ni kweli Harmonize amefunga ndoa bila hata kuhudhuriwa na msanii yeyote kutoka WCB? Ni swali ambalo linakuwa gumu kulijibu.

Kwa upande mwinginbe, Sarah naye pia ameweka video na picha za tukio hilo kwenye Insta Story na hajaziwekea maneno yoyote yale.

View this post on Instagram

BURUDANI :Je, ni kweli Harmonize amefunga ndoa na mchumba wake Sarah?, Hakuna msanii hata mmoja kutoka WCB aliyehudhuria kwenye harusi ————————————————————————————- Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize na mchumba wake Sarah kwa siku ya jana na leo wameendelea kugonga vichwa vya habari hapa Tanzania kwa tukio lao la kufunga ndoa. Swali ni kwamba ni kweli wawili hao wamefunga ndoa? Au kuna kitu kingine kinaendelea. Kwa mujibu wa marafiki wa karibu wa Harmonize wanaopenda zaidi kuweka vitu kwenye mitandao ya kijami, Wamesema kuwa wawili hao jana usiku wamefunga ndoa na ilihudhuriwa na watu wake wa karibu tu ambao anafanya nao kazi kwa sasa. Bongo5 imemtafuta harmonize kuthibitisha taarifa hizo, Lakini namba yake haijapatikana licha ya video nyingi kusambaa mitandaoni zikionesha tukio la sherehe za harusi hiyo. Hata hivyo, Moja ya watu wake wa uongozi wake kwasasa, Ambaye amekataa kutajwa jina, Amesema tukio hilo sio harusi kama inavyodhaniwa bali alikuwa location kwa ajili ya ku-shoot video yake mpya ijayo. Wimbo huo bado haijajulikana lakini huenda ukawa ni ule wa ‘TUWAKOMESHE’ aliomshirikisha Lady Jaydee, Japokuwa bado kuna ukakasi kwani hata Lady Jaydee mwenyewe amempongeza harmonize kwa kufunga ndoa na hakuwepo kwenye tukio. Mwanamitindo maarufu hapa Tanzania, Mustafa Hassanali alikuwa ndio mtu wa kwanza kuposti video ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika, “Hongera sana Sarah kupata Dume. Mungu abarike Ndoa ya Sarah na Rajabu ameen.“. . . . . Kingine, ni kweli Harmonize amefunga ndoa bila hata kuhudhuriwa na msanii yeyote kutoka WCB? Ni swali ambalo linakuwa gumu kulijibu. Kwa upande mwinginbe, Sarah naye pia ameweka video na picha za tukio hilo kwenye Insta Story na hajaziwekea maneno yoyote yale. WRITTEN BY @mgallahtz .

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW