Habari

Je! Unafahamu? Ali Choki alikuwa meneja wa Shetta kipindi yupo darasa la nne!

Leo hii jina la Shetta linasikika ‘loud and clear’ kwenye vyombo vya habari kwa wimbo wake uliotokea kupendwa, Nidanganye aliomshirikisha Diamond.

Lakini kuna mengi usiyoyajua kuhusu kijana huyu aliyezaliwa kwa jina la Nurdin Bilal mwaka 1990. Thanks kwa Spotlight ya East Africa Radio kwa kufanya Bongo5 kujua masuala kadhaa muhimu kuhusiana na mzee wa ‘mdananda’.

1. Akiwa na darasa la nne, mwanamuziki wa dance nchini Ali Choki aligundua kipaji chake na kuamua kuwa meneja wake kwa muda. Kuona hivyo alimpeleka Dogo Shetta studio ili afanye ngoma moja. Chini ya usimamizi wa Choki, kijana akafanya wimbo mmoja uliotengenezwa na Mika Mwamba. Hata hivyo kutokana na wimbo huo kuwa kitoto sana haukumfikisha popote.

2. Kabla hujamjua Shetta huyu wa leo, alikuwa dancer wa Dully Sykes aka Mr. Misifa kwenye crew yake ya Misifa Camp. Kata sana mauno kabla ya kugundua kuwa uwezo wake wa kuchana na kuandika mashairi ni mkubwa kuliko alivyokuwa anafikiria.

3. Akiwa mume wa mtu baada ya kufunga ndoa na Bi. Leyla Yusuf Ali, Shetta alikuwa ameshapata uhakika wa kuwa baba. Alimwoa mke wake akiwa mjamzito tayari. Na sasa ana wiki kadhaa tu ili abadilishe status na kuwa Baba fulani!

4. Alipotoa single yake ‘Nimechokwa’ aliyomshirikisha Belle 9, Shetta alikuwa anatoza laki nane kwa show moja. Baada ya kuachia mdananda akiwa na Dully Sykes na Tundaman akapandisha dau hadi kufikia milioni moja. Na sasa hivi akiwa na single mpya ‘Nidanganye’ bila milioni 2.5 mpaka 3 basi ondoa uhakika wa kumpata kwenye show.

5. Shetta ni muoga sana wa kufulia. Anasema tangu aoe, race za kutafuta mshiko zimeongezeka maradufu ili isije kutokea siku ambayo atashindwa kumpa mkewe mahitaji muhimu. Hapendi kuchekwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents